WAKULIMA WILAYANI KILOSA WALIA NA MASHAMBA YALIYOFUTWA UMILIKI NA RAIS.

Wanachi Kata za Mvumi na Msowero wilayani Kilosa mkoani Morogoro wameiomba serikali kuweka utaratibu wa kuwawezesha kuyatumia mashamba yaliyofutwa umiliki toka kwa wawekezaji na Raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania mwishoni mwa mwaka jana, ambapo wamedai wamekua wakiyategemea kwa kilimo tangu yakiwa chini ya wawekezaji lakini tangu kufutwa kwa umiliki wa mashamba hayo na raisi na kuyarudisha serikalinii ngazi ya wilaya kumekua na sintofahamu juu ya maeneo hayo, hatua inayopelekea wananchi hao kushindwa kuendelea na shughuli zao za kilimo katika mashamba hayo.

Rai hiyo ya wananchi imetolewa wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya wanawake Dunia yaliyofanyika katika Kijiji cha Ludewa- Gongoni wilayani Kilosa yaliyoandaliwa na mtandao wa vikundi vya wakulima nchini (MVIWATA) na kufanikikiwa kuwakutanisha wananchi, Viongozi wa serikali,na wanasheria lengo likiwa ni kujadili changamoto mbalimbali za ardhi zinazowakabili wananchi hao.

Wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu wamekua wakiyatumia maeneo hayo kwa kilimo kwa kupatiwa vibali toka kwa wawekezaji, lakini baada ya Serikali kufuta umiliki hakuna utaratibu maalumu uliowekwa wa kuwawezesha kuyatumia maeneo hayo hatua ambayo inapelekea wananchi wengi kushindwa kufanya shughuli zao za kilimo kutokana na kukosa maeneo ya kilimo.

Kwa upande wake Mwanasheria wa Mtandao wa Wakulima MVIWATA Kuyunga Yango  amesema uwepo wa elimu ndogo kwa wananchi kuhusu sheria ya ardhi inachangia pia wananch wengi kushindwa kujua haki zao hatua inayopelekea wengine kupoteza mali na wengine kulalamika bila kujua utaratibu jinsi ulivyo, huku  akiwataka wananchi hao kuacha kulalamika na babadala yake wafuate utaratibu wa sheria unavyotakiwa ili kuweza kuwasaidia changamoto za mara kwa mara za ardhi zinazotokea katika wailaya hiyo ya Kilosa .

Kwa upande wake mkurugenzi wa MVIWATA ndugu Stephen Ruvuga amesema wameamua kutoa elimu hiyo ya kisheria kwa wakazi wa Kilosa na Mvomero kutokana na maeneo hayo kuwa na changamoto kubwa ya migogoro ya ardhi hivyo wanaungana na serikali ya awamu ya tano chini ya raisi Dr John Pombe Magufuli kuhakikisha wanatokomeza migorogo hiyo kwa njia ya utoaji wa elimu kuhusu sheria ya ardhi pamoja na kutoa msaada wa kisheria kwa wale wote wenye matatizo kuhusu ardhi katika maeneo hayo.

Mgeni rasmi katika ufunguzi huo ambaye umemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr Kebwe Steven, Katibu tawala msaidizi inayesimamia uchumi Ernest Mkongo amesema kwa sasa wanaandaa mpango maalumu wa kuhakikisha mashamba hayo ya wawekezaji yaliyofutiwa kibali na raisi yanagawiwa kwa wananchi huku akipongeza maamuzi ya mtandao wa vikundi vya wakulima MVIWATA kujitokeza katika maeneo hayo na kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi ambao wengi wao hawana uelewa mpana juu ya Sheria.

Kwa upande wake katibu tawala wilaya ya Kilosa ndugu Yohana Kasitila amesema kwa sasa hali imekuwa shwari katika wilaya huku akisema migogoro ya mara kwa mara ya ardhi imepungua kwa kiasi kikubwa  mwaka huu tofauti na miaka mingine, huku akisema jitihida mbalmbali za serikali na wadau wa kilimo ndio imechangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa migogoro hiyo ambayo imekuwa kero wa wananchi.

Kasitila hakuishia hapo bali pia ametoa shukrani za dhati kwa mtandao wa vikundi vya wakuliama MVIWATA kwa kujitokeza na  kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi ambao wengi wao ni wakulima, huku pia akitoa wito kwa mkurugenzi wa MVIWATA kutembea maeneno mengine ndani ya wilaya hiyo ambayo yamekuwa na changamoto hiyo ya ardhi kwa lengo la kuwajengea wigo mpana wa uelewa wananchi.

Wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha Sigara cha Mariboro kilicho kata ya Mkambarani mkoani Morogoro raisi Dr John Pombe Magufuli amesema mashamba hayo ameyafuta kwa lengo la wananchi kugawiwa bure lakini anashangaa mpaka leo bado utekelezaji unasitasita huku akikili uwepo matatizo makubwa ya ardhi katika Mkoa wa Morogoro ikiwemo Kilosa.

Mviwata on Facebook

Subscribe to our monthly newsletter