VIPINDI VYA REDIO KATIKA WILAYA YA KILOMBERO NA ULANGA

MVIWATA, HAKI ARDHI na TAGRODE chini ya mwamvuli wa TALA kupitia mradi wa mpango wa urasimishaji ardhi (LTSP) imefanya vipindi vya redio katika wilaya za Ulanga na Kilombero kwa lengo  la kuelezea masuala mbalimbali yanayohusiana na ardhi pamoja na dhana ya vikundi na mitandao. Vipindi hivyo vilifanyika katika redio ya Pambazuko iliyopo wilaya ya Kilombero  na Ulanga fm iliyopo wilaya ya Ulanga.

Mada zilizojadiliwa katika vipindi hivyo ilikuwa ni Nini maana ya ardhi na mfumo wa utawala wa ardhi ya kijiji, Mfumo wa utatuzi wa migogoro ya ardhi nchini Tanzania, Mpango wa matumizi bora ya ardhi pamoja na Dhana ya vikundi na mitandao. Wakulima walipata nafasi ya kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa kuuliza maswali ambayo yalijibiwa na wanasheria kutoka MVIWATA na HAKI ARDHI pamoja na Mratibu kutoka shirika la TAGRODE.

277 views

Mviwata on Facebook

Subscribe to our monthly newsletter