UFUNGUZI RASMI WA WIKI YA UTOAJI MSAADA WA KISHERIA

Ufunguzi rasmi wa Wiki ya utoaji wa Msaada wa Kisheria umefanyika tarehe 23.10.2019 katika Uwanja wa Ofisi ya Serikali ya Kata ya Chamwino, wenye kauli mbiu “Msaada wa kisheria kwa Maendeleo Endelevu”. Hafla hiyo ilifunguliwa na mgeni rasmi Bi. Neema Haule (Mkurugenzi wa Mashtaka Mkoa wa Morogoro) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Shughuli ya ufunguzi iliandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogogo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo MVIWATA. Shughuli za msaada wa kisheria wiki hii zinaendelea kutolewa katika vituo vinne ambavyo ni Chamwino, Msamvu Stendi kuu ya Mabasi, Mwembesongo na Mawenzi sokoni.  MVIWATA kama mdau muhimu katika utoaji Msaada wa kisheria imeshiriki kutoa Hema ambalo lipo kituo cha Msamvu Stand kuu ya mabasi na wanasheria wawili (2) ambao wanatoa msaada wa Kisheria kwa wiki nzima kuanzia tarehe 21 hadi 25 Oktoba 2019.

241 views

Mviwata on Facebook

Subscribe to our monthly newsletter