KIKAO KATI YA MVIWATA NA WASHAURI ELEKEZI CHA RASIMU YA TATHMINI YA KATI YA UTEKELEZAJI WA MPANGO MKAKATI WA MVIWATA 2017/2021 PAMOJA NA WASHAURI ELEKEZI WA RASIMU YA TATHMINI YA UWEZO WA NDANI WA TAASISI KIMIFUMO KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE.

MVIWATA imefanya kikao jana tarehe 28/5/2019 na Washauri Elekezi wa Kutathmini Rasimu ya Kati ya Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa MVIWATA wa Miaka Mitano 2017-2021 pamoja na Tathmini ya Rasimu ya Uwezo wa Ndani wa Taasisi wa kutekeleza majukumu yake sambamba na mpango mkakati wa Taasisi.

 

Kikao hiki kimefanyika Makao Makuu ya MVIWATA Bigwa Morogoro kikishirikisha Wajumbe wa Bodi ya MVIWATA, Watendaji wa MVIWATA wa Ngazi ya Taifa na Ngazi za Kati za Morogoro, Arusha, Kilimanjaro na Manyara, baadhi ya wanachama wa MVIWATA kutoka Morogoro pamoja na Washauri Elekezi ambao ndio walikuwa wawasilishaji wakuu wa rasimu ya tathmini walizofanya.

 

Washauri Elekezi wameonesha hatua nzuri za Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa MVIWATA ikiwa ni pamoja na Mpango Mkakati kuakisi changamoto za wazalishaji wadogo ikiwemo ukosefu wa uhakika wa ardhi kwa wakulima, changamoto za masoko, huduma rafiki za kifedha pamoja na kilimo endelevu. Vile vile wameainisha changamoto kadhaa ikiwemo kuboresha mifumo ya mawasiliano miongoni mwa wazalishaji wadogo ili kufikia malengo tarajiwa.

Baada ya Kikao na Washauri Elekezi Kikao kiliendelea cha tathmini ya Muda Mrefu miongoni mwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Wanachama na Watendaji wa MVIWATA juu ya mwelekeo wa Taasisi katika Kutetea Maslahi ya Wazalishaji Wadogo na Namna ya Kukabiliana na Changamoto zinazojitokeza.

MWISHO

Mviwata on Facebook

Subscribe to our monthly newsletter