Naibu Waziri Wa Kilimo Mhe. Omari Mgumba amewataka wakulima kuacha kulima kilimo cha mazoea na badala yake wawatumie wataalamu kutoka mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) pamoja na chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine SUA kwa lengo la kupata ujuzi zaidi kuhusu uzalishaji wa mazao yaliyo bora na yenye tija pamoja na masoko kwa lengo la kujikwamua na wimbi la umasikini.
Haya yanabainshwa na naibu waziri huyo wakati akifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Makao Makuu ya Mtandao Wa Vikundi Vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) pamoja na chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine cha SUA Mkoa wa Morogoro, ambapo waziri huyo alijionea shughuli mbalimbali zinafanywa na taasisi hizo ikwemo MVIWATA.
Naibu Waziri Mhe. Mgumba amebainisha malengo ya ziara hiyo katika ofisi hizo za Mtandao Wa Vikundi Vya Wakulima MVIWATA kuwa ni pamoja na kuangalia jinsi mtandao huo wa wakulima unavyotekeleza mpango mkakati wa kilimo yaani ASDP2, kujifunza shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na MVIWATA pamoja na kujadiliana changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo ya kilimo nchini hasa kwa upande wa wakulima.
Katika kutekeleza mpango mkakati wa kilimo yaani ASDP2, naibu waziri Mgumba ameupongeza Mtandao huo wa vikundi vya wakulima MVIWATA kwa kuweza kufanya shughuli zake kuendana na mpango huo huku pia akisifu utendaji wa mtandao huo kuanzia ngazi ya chini mpaka ya juu.
Niabu waziri ameelezea shughuli za MVIWATA kuwa hazina tofauti sana na Ushirika ambao una malengo ya kuwanufaisha wakulima wadogo hapa nchini kwa kuwawezesha wakulima kupata taarifa sahihi za kilimo na masoko, kuongeza ubora wa mazao na vipimo sahihi pale wanapokuwa wakitaka kuuza mazao yao sehemu mbalimbali nchini.
Kupitia mawasilisho yaliyofanywa na MVIWATA katika ziara hiyo, naibu waziri wa kilimo Mhe Mgumba amekiri uwepo wa changamto kubwa katika ardhi kwa kuelezea kuwa zaidi ya asilimia 70% ya ardhi yote nchini inamilikiwa na vijiji lakini Naibu waziri Mgumba anapatwa na hali ya sintofahamu kuhusu umiliki wa ardhi hiyo kwa vijiji kutokana maeneo mengi ya ardhi katika vijiji inamilikiwa na wawekezaji ambao wameshindwa kuendeleza ardhi hiyo hali inayasbabisha ardhi hiyo kuwa mashamba pori.
Katika suala la changamoto la uendeshaji wa masoko yaliyojengwa na MVIWATA katika halmashauri mbalimbali hapa nchini, Mhe naibu waziri Mgumba amekiri uwepo wa upotevu mkubwa fedha ndani ya halmashauri na kusisitiza kuwa mapato yote ya ndani ya halmashauri hayaendi hazina kama inavyobainishwa huku akiahidi kufuatilia fedha zote zilizokubalika kurejeshwa kwenye masoko kwa ajili ya uendeshwaji wa masoko hayo kutokana na sasa
Kabla ya kutembelea ofisi za MVIWATA naibu huyo waziri ametembelea chuo kikuu cha cha Kilimo cha Sokoine SUA kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali za kilimo zinazofanya na chuo hicho, huku akitoa wito kwa taasisi hiyo ya elimu kutoa elimu ya kutosha kwa wakulima kuhusu kilimo cha kisasa na chenye tija kwa lengo la kumnyanyua mkulima kutoka katika wimbi la umasikini kutokana na kulima kilimo cha mazoea.
Mwisho.





