MAPROMOTA 30 KUTOKA MIKOA MITATU YA TANZANIA BARA WAPATIWA MAFUNZO YA UONGOZI NA MVIWATA

Jumla ya wakulima viongozi  thelathini (30) maarufu kama Mapromota kutoka mikoa mitatu(3) ya Tanzania bara ambayo ni Ruvuma, Shinyanga na Morogoro wamepatiwa mafunzo na mtandao wa vikundi vya wakulima  Tanzania (MIVWATA), mafunzo hayo yamefanyika kuanzia tarehe 13/03/2018 mpaka Tarehe 27/03/2018 katika kituo cha mafunzo cha PAUL MAUMBA kilichopo katika kata ya TAWA, Tarafa ya MATOMBO, Wilaya ya MOROGORO VIJIJINI yakiwa na lengo la kuwajengea  uwezo wakulima wadogo katika nyanja mbalimbali ili kuwawezesha na kuboresha uwezo wao wa kutafuta masuluhisho katika changamoto mbalimbali wanazokutana nazo pamoja na kwenda kutoa elimu hiyo na ujuzi walioupata kwa wenzao katika jamii wanakotokea na kuimarisha vikundi na mitandao ya wakulima wadogo ndani ya nchi na kufaidisha wakulima wadogo kiujumla kupitia mabadilishano ya ujuzi.

MVIWATA wametekeleza mafunzo hayo ya Mapromota ikiwa ni mmojawapo wa mpango mkakati wake kwa mwaka 2017- 2021, kulenga kutoa  mafunzo ya uongozi kwa wanachama wake kukiwa na lengo kubwa la kuzalisha wachochea mabadiliko katika jamii za wakulima wadogo ambapo kupitia mafunzo hayo wamejengewa uwezo  ambao nao wataenda kuusambaza kwa wakulima wengine mahali walipotoka kwa lengo kuwa na uelewa mmoja kuhusu masuala mbalimbali ya kilimo nchini.

Zaidi ya wakulima  120  ambao ni wanachama wa MVIWATA  wanategemewa kupatiwa mafunzo hayo ya uongozi (Mapromota) kwa mwaka 2018, huku kuanzia January mpaka March mwaka huu mapromoto 30 tayari washapatiwa mafunzo hayo, kumi na watano wakiwa ni wa kiume(15) na wengine kumi na Watano wakiwa ni wa kike (15) kutoka mikoa mitatu ya Tanzania bara.

Huku katika mafunzo hayo washiriki waliandaa na kuwasilisha mpango kazi katika ngazi ya mkoa  na kupata maoni mbalimbali kutoka kwa muwezashaji wa mada na washiriki wengine kwa maboresho ili kufanikisha ufanisi wa kazi zilizopangwa, pamoja na kubadilishana ujuzi na uzoefu kwa njia mbalimbali za kuimarisha mtandao na kuwezesha elimu ya MVIWATA kwa waliowanachama na wasio wanachama.

Mafunzo hayo ya maparomota yanatarajiwa kuendelea tena  kufanyika kimakundi mwezi Mei mwaka 2018 (NEW INTAKE/BATCH) kwa lengo la kutimiza idadi inayotakiwa kwa mwaka huu wa 2018 huku kwa sasa baadhi ya mapromota wanaendelea na mafunzo ya kisheria kuhusiana na masuala mbalimbali ya ardhi.

MWISHO.

Mviwata on Facebook

Subscribe to our monthly newsletter